Jeremiah 51:11-12


11“Noeni mishale,
chukueni ngao!
Bwana amewaamsha wafalme wa Wamedi,
kwa sababu nia yake ni kuangamiza Babeli.
Bwana atalipiza kisasi,
kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
12 aTwekeni bendera juu ya kuta za Babeli!
Imarisheni ulinzi,
wekeni walinzi,
andaeni waviziao!
Bwana atatimiza kusudi lake,
amri yake juu ya watu wa Babeli.
Copyright information for SwhNEN